Jumatatu, 30 Januari 2017

Rais wa Guinea achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika (AU)


Rais wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais Conde anapokea uongozi kwa Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ni kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the Union). Mwenyekiti huyu huchaguliwa  na Marais wa Nchi wanachama wa AU ambaye hushika wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa zamu katika Kanda tano za bara la Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, na Afrika ya Kati).

Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002 ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza.

Ijumaa, 27 Januari 2017

Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia


Wapiganaji wa al-ShababHaki miliki ya pichaAFP
Image captional-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.
Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa.
CHANZO BBC SWAHILI

ZULU YUPO FITI KUICHEZEA YANGA DHIDI YA MWADUI



KIUNGO wa kimataifa wa Zambia, Justin Zulu yuko fiti kabisa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Mwadui FC, Dar es Salaam.
Yanga watakuwa wenyeji wa Mwadui FC katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili mjini Dar es Salaam, wakihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba kwa sasa kwenye kikosi chao hakuna majeruhi kufuatia kupona kwa Zulu na kiungo mwingine Mzambia, Obrey Chirwa.
Justin Zulu yuko fiti kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Mwadui FC 

Pamoja na hayo, Hafidh alisema mchezaji pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo wa Jumapili ni mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye yuko kwao matatizo ya kifamilia.
“Ni mchezaji mmoja tu ambaye hatupo naye hapa kwa sababu yupo kwao kwa matatizo ya kifamilia, Ngoma. Ila wengine wote wapo na wanaendelea na mazoezi.  
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea wikiendi hii, leo Mbao FC wakiwakaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kesho Simba SC wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Uhuru.
Mechi nyingine za kesho, Tanzania Prisons wataikaribisha Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Toto Africans wataikaribisha African Lyon CCM Kirumba, Mwanza na Ndanda FC na  Maji Maji FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Jumapili mbali na Yanga kuwa wenyeji wa Mwadui FC, Kagera Sugar nao watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar na JKT Ruvu wataikaribisha Stand United.

SOURCE BIN ZUBERY

SIMBA YAMTOA KWA MKOPO BLAGNON OMAN CLUB



SIMBA SC imemtoa kwa mkopo wa miezi sita mshambuliaji wake, Muivory Coast, Frederick Blagnon kwenda klabu ya Oman FC ya Oman.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara alisema jana katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba, Blagnon wameamua kumtoa mkopo mchezaji huyo baada ya kutoridhishwa na dau la Oman Club kumununua moja kwa moja.
“Oman Club hawakuwa na ofa nzuri sana kwa kuwauzia moja kwa moja mchezaji huyo, hivyo tumeona tuwape kwa mkopo kwanza, kama watavutiwa naye na kuongeza dau, tutawapa moja kwa moja,”alisema. 
Frederick Blagnon (kushoto) akiwa kwenye benchi Simba SC

Blagnon anakuwa mchezaji wa pili wa Simba kutolewa kwa mkopo Oman, baada ya mshambuliaji mwingine, mzalendo Daniel Lyanga kutolewa kwa mkopo pia Fanja ya Oman. 
Na wawili hao wanafanya idadi ya jumla ya wachezaji wa Simba wanaocheza kwa mkopo kufika watano, baada ya wengine watatu kutolewa kwa mkopo kwenye timu mbalimbali za hapa nyumbani.
Hao ni beki Emmanuel Semwanza aliyepelekwa Maji Maji ya Songea na viungo 
Awadh Juma aliyepelekwa Mwadui FC ya Shinyanga na Peter Mwalyanzi aliyepelekwa African Lyon ya Dar es Salaam.
Blagnon alijiunga na Simba SC kwa dau la Sh. Milioni 100 kutoka African Sports ya kwao, Ivory Cioats Julai mwaka jana, lakini pamoja na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubw azaidi kikosini, akashindwa kuonyesha thamani yake.

CHANZO BIN ZUBERY

WAZUNGU WAMUOMBEA ITC ULIMWENGU AANZE KAZI SWEDEN




KLABU ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden imemuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu tayari kuanza kumtumia baada ya kumsajili.
Tangu juzi Ulimwengu yuko Hispania na klabu yake hiyo mpya, AFC Eskilstuna kwa maandalizi ya Ligi Kuu ya Sweden. 
Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema kwamba AFC Eskilstuna imekwishaomba ITC ya Ulimwengu. “Tayari tumepokea maombi ya ITC ya Ulimwengu kutoka klabu ya AFC Eskilstuna,”alisema Lucas. 


Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya Athletic FC ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.
Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na  Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.

source bin zubery

Tanzania na Malawi kujadiliana kuhusu Watanzania waliokamatwa nchini humo

Tume ya Ushirikiano wa Pamoja ya Kudumu (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi, inatarajia kukutana nchini humo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo la Watanzania nane kukamatwa nchini humo kwa tuhuma za kuingia eneo la migodini bila kuwa na kibali.
 Mbali na kujadili suala la Watanzania hao, lakini pia tume hiyo itajidili mgogoro wa mpaka uliopo baina ya nchi hizo mbili katika Ziwa Nyasa. 

Mkutano huo unatarajiwa kuanza Februari 3 hadi 5 mwaka huu nchini Malawi. Akizungumza Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga alisema tume hiyo ilikuwa haijakutana kwa muda mrefu, jambo ambalo limesababisha watu kuwa na sintofahamu kati ya ushirikiano wa nchi hizo mbili
 Kasiga alisema mkutano wa tume hiyo, mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2003 jijini Dar es Salaam, hivyo kuwa kimya kwa muda mrefu kuna baadhi ya watu walidhani kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili si mzuri. “Kikao kama hiki kilikaa miaka mingi kidogo…

 kuna masuala yaliyochelewa kutekelezwa kutokana na kukaa kwa kikao hiki, lakini kwa sasa yatatekelezwa kupitia vikao hivyo,” alisema Kasiga. Aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza, vikao hivyo vitashirikisha wafanyabiashara kutoka mikoa ya Njombe na Ruvuma, pia wavuvi kutoka katika mikoa hiyo ambao wataeleza namna wanavyofanya shughuli zao kwa kushirikiana na wenzao wa Malawi bila kuingilia.

 Mindi alisema katika kikao hicho, ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga; na mbali na kujadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Watanzania waliokamatwa, pia utajadili masuala mbalimbali katika sekta za biashara, elimu, kilimo pamoja na sekta zingine. Kasiga pia alikabidhi tuzo za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walizoshinda kutoka Umoja wa Afrika (AU).

 SSRA ambayo imekuwa wa kwanza katika Tuzo za Ubunifu Katika Sekta za Umma Afrika (AAPSIA), ilikabidhiwa kikombe pamoja na cheti cha ushindi. Ushindi huo wameupata kupitia mradi wao wa Mradi wa Kanzidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.