Jumamosi, 4 Februari 2017

Picha mmiliki wa taharuki blog(katikati) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa bbc media action

KARIBU LIGI KUU LIPULI....

CHANZO SALEHE JEMBE

Lipuli imeitwanga Polisi kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kurejea Ligi Kuu Bara.

Ushindi wa Liipuli unaifanya Lipuli imeitwanga Polisi kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kurejea Ligi Kuu Bara.


TAIFA STARS YAPEWA AMAVUBI KUFUZU CHAN 2018 KENYA

TANZANIA itaanza na Rwanda katika kuwania tiketi ya Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2018 nchini Kenya.
Hiyo ni itakuwa katika Raundi ya pili ya mchujo wa michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee na Taifa Stars itaanzia nyumbani Dar es Salaam kabla ya kuwafuata Amavubi Kigali. 
Mechi nyingine kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zitakuwa ni kati yaa Uganda na mshindi baina ya Somalia na Sudan Kusini zitakazomenyana katika Raundi ya Awali ya mchujo kati ya Aprili 20, 21 na 22 mwaka huu na kurudiana na kati ya Aprili 28, 29 na 30.
Djibouti itamenyana na Ethiopia, wakati Burundi itamenyana na Sudan na mechi za kwanza zinatarajiwa kufanyika kati ya Julai 14, 15 na 16 mwaka huu, wakati marudiano yatakuwa kati ya Julai 21, 22 na 23.
Ikifanikiwa kuitoa Rwanda, Tanzania itamenyana na mshindi kati ya Uganda na ama Sudan Kusini au Somalia katika Raundi ya Tatu ya mchujo mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Agosti 11, 12 na 13 na marudiano kati ya Agosti 18, 19 na 20, mwaka huu.
Tanzania imewahi kushiriki mara moja tu fainali za CHAN, ambayo ilikuwa ni mwaka 2009 zikifanyika kwa mara ya kwanza kabia.

SAMATTA AWATOA HOFU KRC GENK JUU YA MAUMIVU YAKE

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba maumivu ya mgongo aliyoyapata Februari 1, mwaka huu hayatamuweka nje kwa muda mrefu, sana wiki moja tu. 
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Genk, Samatta alisema kwamba kwa sasa anaendelea vizuri na anatarajia wiki ijayo ataanza mazoezi.
“Yalikuwa ni maumivu kidogo, ambayo sana nitakaa nje kwa wiki moja. Itategemea na jinsi nitakavyokuwa napata ahueni,”alisema.
Mbwana Samatta amesema kwamba anatarajia kurejea uwanjani wiki ijayo baada ya kupona maumivu ya mgongo 

Usiku wa Februari 1, Samatta alicheza kwa dakika 23 tu kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akiiacha timu yake, KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende Uwanja Luminus Arena, Genk katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji na kutolewa.
Samatta aliumia dakika ya 23 na kulazimika kumpisha Mspaniola Jose Naranjo ambaye alikwenda kukosa penalti na bao la Mzimbabwe, Knowledge Musona dakika ya nane likaimaliza Genk.
Huo ni mchezo wa pili mfululizo KRC Genk inapoteza, baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita pia kuchapwa 1-0 na KV Mechelen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji. 
Siku hiyo Samatta alicheza kwa dakika zote 90 jana Uwanja wa ugenini wa AFAS Achter de Kazerne mjini Mechelen na bao pekee la beki Mbelgiji, Seth De Witte dakika ya 89 likawapa wenyeji ushindi wa 1-0.
Tayari Samatta amecheza mechi ya 40 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 22 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 21 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 10 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 11, matano msimu huu na sita msimu uliopita.

SIMBA YAFANYA MAUAJI SONGEA, YAILIPUA MAJI MAJI 3-0

SIMBA SC imejirudisha jirani kabisa na mahasimu wao, Yanga SC katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 jioni ya leo dhidi ya wenyeji Maji Maji, Uwanja wa Maji Maji Songea mkoani Ruvuma.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 21, sasa wakizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga. 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ahmed Kikumbo wa Doodma, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Ibrahim Salum Hajib Migomba dakika ya 19, hilo likiwa bao lake la nne msimu huu akiunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya winga Shiza Ramadhani Kichuya.
Katika kipindi hicho, Simba ilitawala vizuri mchezo na kama washambuliaji wake wangekuwa makini wangetoka wanaongoza kwa mabao zaidi.
Nafasi pekee nzuri ambayo Maji Maji waliipata wakashindwa kuitumia ilikuwa ni dakika 45 baada ya Marcel Bonaventura kupiga vizuri shuti la mpira wa adhabu, ambalo kipa wa Simba, Mghana, Daniel Agyei alitema mpira mbele ya Kevin Kibuta na Suleiman Kibuta, lakini wakashindwa kuurudisha nyavuni hadi ukaokolewa.
Kipindi cha pili, Simba ya kocha Mcameroon Joseph Marius Omog iliendelea kung’ara na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi, hivyo kuizima kabisa Maji Maji.
Kiungo mwenye kipaji kikubwa, Said Hamisi Ndemla aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 63 kwa shuti baada ya kona chini chini ya kiungo Mghana, James Kotei aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Pamoja na kufungwa, Maji Maji walio chini ya kocha Muingereza mwenye asili ya Kongo aliyezaliwa Tanzania, Kali Ongala waliendelea kucheza vizuri wakitengeneza nafasi, lakini hazikuwa za maana. 
Zikiwa zimesali dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho, mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 88 akimvisha kanzu beki baada ya pasi ya kichwa ya kiungo Mwinyi Kazimoto aliyetokea benchi.
Bao hilo liliimaliza kabisa Maji Maji na kutoka hapo wakawa wanacheza ili mechi iishe. Huu ni ushindi wa kwanza wa Simba katika Ligi Kuu mwaka huu, baada ya awali kutoa are bya 0-0 na Mtibwa Sugar na kufungwa 1-0 na Azam FC.
Kikosi cha Maji Maji kilikuwa; Hashim Mussa, Saleh Abdallah, Mpoki Mwakinyuke, Emmanuel Semwanza, Kennedy Kipepe, Alex Kondo, Iddi Kipwangile, Hassan Hamisi, Suleiman Kibuta/George Pole dk84, Marcel Bonaventure/Luka Kikoti dk73 na Kelvin Sabato. 
Simba SC; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Novatus Lufunga, Method Mwanjali, Muzamil Yassin, Shiza Kichuya, Said Ndemla/Mwinyi Kazimoto dk76, Laudit Mavugo, Juma Liuzio/Pastory Athanas dk52 na Ibrahim Hajib/James Kotei dk59.

Ijumaa, 3 Februari 2017

Wananchi shirikianeni NA polisi ili kumaliza ubakaji

Wito umetolewa kwa wananchi kushirikiana Na jeshi LA polisi wilayani Mbulu ili kuweza kutokomeza tatizo LA ubakaji wilayani hapa.

Wito huo umetolewa NA mkuu Wa wilaya ya Mbulu mkoani manyara ndugu chelestino mofugawakati akizungumza NA Redio habari njema akiwa ofisini kwake

Amesema kesi nyingi za ubakaji zinashindwa kufanikiwa kutokana NA wananchi kutoweza kutoa ushirikano kwa polisi pindi inaporipotiwa kesi ya ubakaji .

Tatizo LA ubakaji limekuwa sugu hapa wilayani Mbulu NA kwa mwaka 2016 zimeripotiwa kesi 22 idadi hiyo kuonesha tatizo kuongezeka kila mwaka .

By Agustino Hamis

Mahojiano ya mwandishi Wa habari Wa kituo cha Redio habari njema Sista Editha temu NA mkuu Wa wilaya ya Mbulu ndugu chelestino mofuga. Picha Na mpiga picha wetu