Jumanne, 11 Aprili 2017




Staa wa soka wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool ya England Sadio Mane leo Jumanne ya April 11 2017 amefanyiwa upasuaji wa goti lake la kushoto.









Juventus wameiadhibu FC Barcelona robo fainali ya UCL






Baada ya mapumziko mafupi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa April 11 2017 mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya Juventus dhidi ya FC Barcelona ulichezwa mjini Turin wakati mchezo wa Borussia Dortmund dhidi ya Monaco ukiahirishwa hadi April 12 saa 19:45 EAT kwa sababu za kiusalama.
Mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Juventus nchini Italia ulianza kuibeba Juventus kuwa na rekodi ya kutowahi kufungwa na Barcelona katika ardhi ya Italia, wakiwa wamewahi kutoka sare mara mbili na Barcelona kupoteza mara mbili wakati mara ya mwisho kukutana ilikuwa Berlin katika mchezo wa fainali UEFA Champions League 2015 na Juventus akapoteza kwa magoli 3-1.
Juventus wakiwa Turin katika mji wao na sapoti kubwa ya mashabikiwa wao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yakifungwa na Paulo Dybala dakika ya 7 na 22 na goli la mwisho likafungwa na Giorgio Chiellinidakika ya 55, Juventus na Barcelona watacheza mchezo wa marudiano April 19 Nou Camp.

MAKUBWAAA

ULU

Kiongozi wa kimila katika Kijiji cha Endagulda ameamriwa akamatwe baada ya kuitoza faini maiti.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Chelestino Mofuga aliagiza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kiongozi huyo.

Mofuga ametoa agizo hilo juzi kijijini hapo baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kuwa, mzee wa kimila, Joseph Daniel aliagiza Gadii asizikwe hadi faini hiyo itakapolipwa.

Awali, kiongozi huyo wa kijiji aliagiza kulipwa faini ya ng’ombe mmoja kutoka kwenye zizi la marehemu Boay Gadii (42) kabla ya maziko yake ikielezwa kuwa alitengwa na jamii.



Auawa kwa kuwa mfugaji wa ng'ombe India

Azmat ni mkulima wa ngombe za m,aziwa aliyepigwa hadi kufa
Image captionAzmat ni mkulima wa ngombe za m,aziwa aliyepigwa hadi kufa
Muislamu mmoja nchini India amefariki kutokana na majeraha aliopata baada ya kundi moja la wanaume waliokuwa wakisafirisha ng'ombe kushambuliwa na wanachama wa kundi moja linalodaiwa kulinda ng'ombe.
Kulingana na ripota wa BBC Nitin Srivastava aliyesafiri hadi katika kijiji cha mwathiriwa cha Jimbo la kaskazini la Haryana, wanakijiji walikuwa wakipigania kumuona kijana huyo aliyetoka hospitalini.
Azmat ambaye hutumia jina moja pekee amejifunika nguo , huku akiwa na jeraha la mbavu, damu katika jicho lake la kushoto mbali na majeraha ya kushambuka katika mikono yake na tumbo.
Hatahivyo ana bahati ya kuwa hai.
Azmat pamoja na watu wengine wanne walishambuliwa na walinda ng'ombe wakati walipokuwa wakisafirisha ng'ombe walizonunua kutoka Jaipur katika jimbo la kaskazini la Rajasthan wakielekea katika shamba lao la ng'ombe wa maziwa huko Hiryana.
Ng'ombe nchini IndiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNg'ombe zinadaiwa kuwa takatifu nchini India
Licha ya kuwa na vibali halali walitolewa katika barabara kupigwa na fimbo huku umma ukitaka wachomwe wakiwa hai.
''Iwapo polisi hawangefika na kutuokoa sote tungekuwa tumefariki ,aliambia BBC Hindi''.
Ngombe hutambulika kuwa mnyama mtakatifu na raia wa dini ya Hindu walio wengi na kwamba mauaji ya ngombe ni haramu katika majimbo mengi ya India.
Mwezi uliopita ,jimbo la Gujarat lilipitisha sheria inayoharamisha uchinjaji wa ng'ombe na kwamba wanaopatikana wakifanya hivyo watapewa kifungo cha maisha

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.

moja ya meli kubwa za kivita zinazomilikiwa na marekani zinazobeba ndege kubwa za kivita
Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Bwana Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini bila ya Uchina.
Bwana Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa.
Marekani imetuma meli za kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea hatua ambayo imeighadhabisha Korea Kaskazini

Simba Sports Club

Dar es salaam,Tanzania
11-4-2017.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Leo mchana huu kunatembea taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.
Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano.
Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari,pia waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale,,ni kushangazwwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu,Hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.
Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha
Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
IMETOLEWA NA..
Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
*SIMBA NGUVU MOJA*