Jumanne, 23 Mei 2017

MKWASA ANENA

Kauli ya Mkwasa 
Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kujizurulu mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji baada ya kupokea rasmi nakala ya barua ya kujiuzulu.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kupokea nakala ya barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji, amesema amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Mapema Mkwasa alikanusha habari hizo ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii lakini baada ya ofisi yake kupokea nakala ya barua hiyo mchana huu, amelizungumzia jambo hilo kwa uchungu na kuwataka mashabiki , wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuwa watulivu mpaka hapo klabu itakapoa tamko rasmi kutokana na taarifa hiyo.
Barua ya kujiuzulu Yusufu Manji amemwandikia makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga na nakala kutumwa kwa raisi wa TFF, bodi ya wadhamini Yanga SC na ofisi ya katibu mkuu Yanga Afrika.
” ni kweli mwanzo sikupata taarifa hizi lakini baada ya kupokea nakala niseme wazi nimesikitishwa na kitendo hiki lakini hatuwezi kupingana na taarifa hiyo. Barua inaeleza afya yake kuzorota na ameshauriwa kupata muda mwingi wa kupumzika hivyo hatoweza kuendelea na majukumu ya klabu na hata ofisini kwake ametoka mpaka hapo afya yake itakapo tengemaa” alieleza Boniface Mkwasa.
Mkwasa amefafanua zaidi kwa kusema suala hilo lipo katika mamlaka ya makamu mwenyekiti hivyo atalitolea ufafanuzi na tamko rasmi kwa wanachama baada ya kikao maalumu cha uongozi kujadili ombi hilo la mwenyekiti kujiuzulu ila kwa sasa kikatiba Clement Sanga ambaye ni makamu mwenyekiti atakaimu nafasi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni