Yanga watangulia Dodoma
- Updated: May 23, 2017
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo klabu ya Yanga, alhamis wanatarajia kueleke mkoani Dodoma kupeleka Kombe la Ligi Kuu kwa wakazi wa mkoani humo.
Yanga na Polisi Dodoma zilitarajiwa kucheza mchezo huo siku ya Alhamis lakini sasa mchezo huo hautafanyika kufuatia wamiliki wa uwanja huo kuufunga kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho siku ya Jumamosi kati ya Simba SC na Mbao FC.
Kuwepo mchezo huo kabla ya mechi ya fainali, kulionekana kuongeza presha kwa watani wake Simba SC ambao waliona Yanga inakwenda kutia mkono wake Dodoma kuelekea mchezo wa fainali jumamosi.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema mchezo huo wa kirafiki ulikuwa ni sehemu ya mualiko wa waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wanaondelea na vikao vya bejeti 2017-18 na wakazi wote wa Dodoma kupata nafasi ya kuiona timu yao ikiwa na kombe la Ubingwa.
Aidha Mkwasa amesema baada ya Dodoma, Yanga itaelekea mkoani Arusha kwa mchezo mwingine wa kirafiki na kulionyesha kombe lake kwa wakazi wa kanda hizo, kabla ya kurejea Dar es salaam na kutoa mapumziko kwa wachezaji wake kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017-18.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni