Ijumaa, 30 Juni 2017

organized-closet
Mara nyingi unaweza kukuta mtu ana kabati limejaa nguo hadi zinakosekana pa kuwekwea na katika hali halisi anajiona hana nguo za kuvaa. Hali  hii inatokana na kukosa mpangilio wa nguo kwenye kabati na pia kuweka nguo ambazo hazihitajiki tena. Nguo zisipokuwa na mpangilio maalumu ni ngumu sana kutafuta nguo gani uivae na ipi maana hujui ipo upande gani wa kabati. Pia pale unapohifadhi nguo ambazo unajua hutazivaa tena inasababisha kabati kujaa bila sababu. Njia hizi zitakusaidia katika kupanga kabati lako:
1. Tafuta siku ambayo unamuda wa kutosha na toa nguo zako zote kabatini kisha tenga zile ambazo unahitaji kuzivaa na zile ambazo unaona hutazivaa tena ( iwe zimekubana, zimechakaa, hauzitaki tena n.k).
2. Tafuta mfuko safi uweke nguo zote ambazo hutazivaa tena ambazo upo tayari kugawa kwa wenye uhitaji. Ni vyema ukianzia nyumbani mwako, kama una dada wa kazi unaweza mpa zile ambazo zitamfaa na kisha nyingine ukapelekea wengine wenye mahitaji unaowafahamu kama ni kanisani au mahali popote pale. Ila jihadhari usimpe mtu nguo iliyochakaa sana, haipendezi.
3. Nguo ambazo unazihitaji zitenge katika makundi (blauzi, sketi, magauni, n.k) na kisha uzikunje vizuri na kuzipanga kabatini kila kundi sehemu yake. Hii itakusaidia ukiwa unatafuta gauni unajua uangalie sehemu gani.  Nguo zinazoendana pamoja kama suti au vitenge ni vyema zikawekwa pamoja sketi na blauzi yake. Kama kabati lina nafasi kubwa makoti ya suti yakiwekwa kwenye henga yanapendeza zaidi.
4. Vitu kama mikanda, skafu, mitandio n.k viwekwe mahali pake ili iwe rahisi kupatikana pale vinapohitajika.

Jitahidi uwe na tabia ya kupanga nguo zako kila unapozifua. Ilikuepuka kutafuta nguo asubuhi na hatimaye kuharibu mpangilio wa kabati lako ni vyema kama utakuwa na utaratibu wa kunyoosha nguo za wiki zima kila mwisho wa wiki, hii itaokoa muda na ‘stress’ za kutafuta nguo ya kuvaa kila asubuhi.

by AGUSTINO HAMIS 

Wanachama Wa chama cha waandishi Wa habari Manyara wakiwa katika mkutano mkuu Wa chama hicho katika ukumbi Wa community center Mbulu mjini


Jumanne, 23 Mei 2017


HABARI

Nape: Niliunda kamati kuchunguza tukio la uvamimizi, sio RC


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kamati aliyounda ilikuwa kwa ajili ya kuchunguza tukio la uvamimizi wa Clouds Media na sio RC wa Dar es Salaam.

Nape Nnauye
Ukupitia mtandao wa twiter Nape ameandika, ‘Niliunda Kamati Kuchunguza tukio la kumamiwa kituo cha utangazaji sio kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayupo juu ya sheria!.

Hiyo jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa Star Tv kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi alikana tuhuma zinazomkabali kuhusu uvamizi na kuongeza kuwa kamati iliyoundwa haikuwa na mamlaka ya kumuhoji.
“Sijawahi kuvamia kituo chochote kile cha runinga , nafasi yangu kama mkuu wa mkoa naweza kumuita mtu yoyote, nina maswali kama 50 kwenye lile neno ‘Kuvamia’ la kwanza wanasema nilivamia kipindi kirushwe wakati kipindi kile kilikuwa kiko live, Watanzania kama hapa tuko live hivi mtu unaweza kuvamia kweli wakati tuko live.” alieleza.

HABARI

Rais wa Korea Kusini afikishwa mahakamani kuanza kesi




Baada ya kukamatwa mwezi machi mwaka huu na kushitakiwa makosa mbali mabali ikiwemo la rushwa mwezi April mwaka huu, hatimaye Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.

Park Geun-Hye alifikishwa mahakamani
Park mwenye miaka 65, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza akiwa mahakamani hapo na rafiki wake wa karibu Choi Soon-Sil, tangu aondolewe madarakani.Park anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa makubwa nchini humo.
Park Geun-Hye aliwa amekaa upande wa kushoto na amevalia ngua ya dark blue huku Choi Soon-Sin akiwa amekaa kulia na amevalia ngua kama nyeupe.
Park alipokuwa mahakanai aliulizwa swali kuwa akjira yake ni nini na nakajibu han na ahajaariwiwa,Rais Park na rafiki yake Bi Chai hawakuongea chochote na waandishi bali walikaapembemni na mawakili wao na kuzungumza na hao tu, hata wawili hao wahakuvaa sare za wafungwa kama walizovaa wakiwa garezani ila walivaa mavazi ya kawaiada.
Park ndiye rais wa tatu wa zamani Korea Kusini kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu, shirika la habari la Yonhap limeripoti.

Twiga yaendelea na mazoezi



Wachezaji wa Twiga Stars wanaendelea na Mazoezi kwenye uwanja wa Karume, wakiwa chini ya kocha Mkuu Sebastian Nkomwa.

BY HAMZA FUMO

BURUDANI


Sijawahi kuwa teja wa dawa za kulevya – Young Dee





Baada ya uliokuwa uongozi wa zamani wa Young Dee ‘MDB’ kudai waliachana na rapa huyo kwa madai ya kurudia kutumia dawa za kulevya, Yound Dee amedai hajawahi rudia kutumia dawa za kulevya huku akidai yeye hakuwahi kuwa muathirika wa dawa za kelevya. Pia rapa huyo amefunguka kuhusu familia yake, uongozi wake mpya pamoja na wazani.

BURUDANI


Hii ndio ngoma iliyomtangaza zaidi Joh Makini kimataifa


Mkali wa muziki wa Hip Hop kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amesema kolabo yake na AKA ‘Don’t Bother’ imemtangaza zaidi kimataifa na kumpa heshima.

Joh Makini na AKA
Joh makini amesema kolabo hiyo imemuongezea thamani na imemtambulisha nje kwa kiwango kikubwa sana, mpaka anapata air time kwenye nchi kama South Africa na watu wanamjua kwa kiwango fulani, ni kwa sababu ya kolabo hiyo.
“Ukitaja wasanii ambao wapo mainstream pale South Africa huwezi kuacha kumtaja AKA, kiasi kwamba hata wasanii wa pale kumpata kwa kolabo inakuwa ni ngumu,” Joh Makini ameimbia Clouds Fm na kuongeza.
“Kufanya kazi na mtu kama yule kwanza inakutengenezea Respect alafu inaonyesha userious ulionao na watu lazima waheshimu hilo, unapofanya kazi wasikuchukulie poa. Hatujawahi kuongea kwamba tutoe ngoma yake au yangu pengine siku za mbeleni,” amesema Joh Makini.

HABARI


Mwanamke India aweka rekodi kuupanda mlima Everest


Anshu Jamsenpa amekuwa mwanamke wa kwanza kuupanda mlima Everest hadi kufikia kileleni katika siku tano.
Jamsenpa ambaye ana umri wa miaka 37 ni mama wa watoto wawili, alifika kileleni mwa mlima huo Jumanne ya Mei 16 wiki iliyopita na alirejea tena chini Jumapili hii.
Mama huyo amekuwa mwanamke wa kwanza kutoka nchini India kufika katika kilele cha mlima huo.
Taarifa hizo zimefika wakati wapanda milima wapatao watatu wamefariki dunia ndani ya wiki moja akiwemo mmoja kutoka Australia alifariki akipanda mlima huo kutoka upande wa Tibet, naye raia wa Slovakia na mmoja kutoka Marekani walifariki dunia katika upande wa Nepal.
Maafisa wa uokoaji wameshindwa kumfikia mpanda milima wa nne, ambaye anatoka India, na ambaye alitoweka muda mfupi baada ya kufika kileleni.

KUTOKA WCB

BURUDANI

Kama hujui kuandika nyimbo WCB hupati nafasi – Diamond



Rais wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amefunguka na kusema ni vigumu kwa msanii kujiunga na lebo yake hiyo kama hajui kuandika nyimbo.

Rayvanny, Rich Mavoko, Diamond, Queen Darleen na Harmonize
Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa wimbo unapoandikwa ndani ya lebo hiyo mara zote unakaguliwa na watu wote ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.
Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa,” amesema Rich Mavoko na kuongeza.
Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

Yanga watangulia Dodoma

Yanga watangulia Dodoma 

Kikosi cha Yanga
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo klabu ya Yanga, alhamis wanatarajia kueleke mkoani Dodoma kupeleka Kombe la Ligi Kuu kwa wakazi wa mkoani humo.
Yanga na Polisi Dodoma zilitarajiwa kucheza mchezo huo siku ya Alhamis lakini sasa mchezo huo hautafanyika kufuatia wamiliki wa uwanja huo kuufunga kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la  Shirikisho siku ya Jumamosi kati ya Simba SC na Mbao FC.
Kuwepo mchezo huo kabla ya mechi ya fainali, kulionekana kuongeza presha kwa watani wake  Simba SC ambao waliona Yanga inakwenda kutia mkono wake Dodoma kuelekea mchezo wa fainali jumamosi.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema mchezo huo wa kirafiki ulikuwa ni sehemu ya mualiko wa  waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wanaondelea na vikao vya bejeti 2017-18 na wakazi wote wa Dodoma kupata nafasi ya kuiona timu yao ikiwa na kombe la Ubingwa.
Aidha Mkwasa amesema baada ya Dodoma, Yanga itaelekea mkoani Arusha kwa mchezo mwingine wa kirafiki na kulionyesha kombe lake kwa wakazi wa kanda hizo, kabla ya kurejea Dar es salaam na kutoa mapumziko kwa wachezaji wake kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017-18.

MKWASA ANENA

Kauli ya Mkwasa 
Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kujizurulu mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji baada ya kupokea rasmi nakala ya barua ya kujiuzulu.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kupokea nakala ya barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji, amesema amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Mapema Mkwasa alikanusha habari hizo ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii lakini baada ya ofisi yake kupokea nakala ya barua hiyo mchana huu, amelizungumzia jambo hilo kwa uchungu na kuwataka mashabiki , wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuwa watulivu mpaka hapo klabu itakapoa tamko rasmi kutokana na taarifa hiyo.
Barua ya kujiuzulu Yusufu Manji amemwandikia makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga na nakala kutumwa kwa raisi wa TFF, bodi ya wadhamini Yanga SC na ofisi ya katibu mkuu Yanga Afrika.
” ni kweli mwanzo sikupata taarifa hizi lakini baada ya kupokea nakala niseme wazi nimesikitishwa na kitendo hiki lakini hatuwezi kupingana na taarifa hiyo. Barua inaeleza afya yake kuzorota na ameshauriwa kupata muda mwingi wa kupumzika hivyo hatoweza kuendelea na majukumu ya klabu na hata ofisini kwake ametoka mpaka hapo afya yake itakapo tengemaa” alieleza Boniface Mkwasa.
Mkwasa amefafanua zaidi kwa kusema suala hilo lipo katika mamlaka ya makamu mwenyekiti hivyo atalitolea ufafanuzi na tamko rasmi kwa wanachama baada ya kikao maalumu cha uongozi kujadili ombi hilo la mwenyekiti kujiuzulu ila kwa sasa kikatiba Clement Sanga ambaye ni makamu mwenyekiti atakaimu nafasi hiyo.

Kunani Kagera Sugar?

Kunani Kagera Sugar?


Lazima klabu kama Kagera Sugar na Tanzania Prisons na hata JKT Ruvu zijiulize sana kwanini timu zingine zinapata udhamini halafu wao wapo wapo tu.
Stand United wamekuja kwenye ligi wakapata deal ya bin slum na baadae ya acacia.
Mbeya city wamekuja wamepata deal ya bin slum wana ya coca cola na sasa wana hii sportsmaster cjui
Singida kaja amepata patnership na NMB na leo Sportpesa
Timu zote hizi zimezikuta Kagera Sugar, Tanzania Prisons na JKT Ruvu ambazo kwa pamoja na simba na yanga zimedumu kwenye ligi kwa muda mrefu
Ni wakati wa hizi timu kujitathmini na kukaribisha mawazo mapya ya kuzisogeza mbele kagera wana wachezaji wazuri wana kocha mzuri wamemaliza msimu nafasi ya tatu wakipata changamoto mpya wanaweza hata kuwania ubingwa namaanisha kuwania sio kutwaa kwa achievement ya msimu huu wanaweza kabisa.
Mbao FC wameingia ligi kuu msimu huu na kulamba mkataba mfupi na Cowbell sambamba na Ruvu Shooting wakiwaacha wakongwe kibao . Ni dhahiri kujitathimini kunahitajika kwa kiwango kikubwa
.

Lwandamina atoa mustakabli wa usajili mpya msimu ujao

Lwandamina atoa mustakabli wa usajili mpya msimu ujao


George Lwandamina kocha mkuu Yanga SC amesema kikosi chake cha Yanga SC kinahitaji mabadiliko makubwa kuendana na hadhi ya klabu hiyo kitaifa na kimataifa.
Baada ya kuvunja kambi rasmi atakabidhi ripoti nzima ya ligi kwa uongozi na kwa ushirikiano watajua jinsi gani watakiboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa ligi Tanzania 2017-18 utakaoanza mwezi August mwaka huu.
Yanga SC wanatarajiwa kuvunja rasmi kambi yao wiki ijayo baada ya ziara yao mikoani inayoanza rasmi kesho. Kesho wataondoka mapema jijini Dar kuelekea Dodoma na mwishoni mwa wiki watakuwa jijini Arusha .
Yanga SC wameibuka mabingwa wa ligi kuu msimu huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo 2014-15,2015-16 na msimu huu 2016-17.
Kipindi chote cha msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara Yanga licha ya kuibuka mabingwa lakini bado walikuwa wakionesha udhaifu nafasi mbalimbali katika kikosi chao.
Kiungo cha chini limekuwa tatizo sugu katika kikosi hicho toka alipokuwepo bwana Hans Van Pluijm . Licha ya utitiri wa viungo katika klabu hiyo lakini bado hawajapata mtu sahihi kuiendesha vyema timu eneo hilo. Kuondolewa kwa Mbuyu Twite na kuletwa Justine Zulu toka Zesco United bado hakujatibu tatizo hilo sugu ambalo lilianza mara baada ya viungo Athuman Chuji na Frank Domayo kuondoka katika kikosi hicho.
Justine Zulu majeraha ya mara kwa mara na kukosa match finess kwa kipindi kirefu kumemfanya kucheza chini ya kiwango pia kukosekana mara kwa mara kwenye kikosi hicho. Juma Saidi ‘ Makapu ‘ aliyeanza kukuzwa vyema na Maximo katika kikosi hicho bado hajalitendea haki eneo la kiungo cha chini . Mara nyingi amekuwa akipanda na kushuka katika kiwango chake pia majeraha ya mara kwa mara.  Muunganiko wa viungo wachezeshaji Haruna Niyonzima na Thabani Kamusoko ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi zote za kiungo , wamegeuka msaada mkubwa kuisaidia nafasi hiyo. Hivyo ni dhahiri Lwandamina anakwenda kuliangalia upya eneo hili ili awe imara na kikosi chake msimu ujao.
Beki ya kushoto ya timu hiyo imekuwa ikimtegemea zaidi Haji Mwiji na mbadala wake Oscar Joshua kuonekana umri unamtupa mkono na kasi yake kupungua . Mara nyingi Mwinyi akiwa mgonjwa au kuchoka kutokana na fatigue timu inayumba katika nafasi hiyo . Hivyo ni dhahiri Lwandamina ataliangalia pia eneo hilo.
Safu ya walinzi wa kati wanaposimama Nadir Haroub , Vincent Andrew, Kelvin Yondani na Vicent Bossou napo panahitaji jicho la kipekee . Nadir mwenye miaka 11! katika kikosi hicho anaonekana kuanza kuchoka sanjari na pacha wake Kelvin Yondani ambaye nae umri umesogea ingawa bado uwezo upo . Lwandamina anahitaji damu changa yenye kasi na uchu wa mafanikio kwa ajili mustakabali mpya wa klabu hiyo kwa miaka mitatu au mitano ijayo.
Wing ya kulia ya timu hiyo amebaki Saimoni Msuva tu katika ubora wake na mara kwa mara tumeona akiumia timu inapwaya na kukosa mtu wa kaliba yake. Juma Mahadhi aliyesajiliwa msimu huu amekosa mwendelezo mzuri wa kipaji chake katika timu hiyo. Ana uwezo wa kucheza kama winga wa kulia na kiungo mshambuliaji lakini mara kwa mara kapewa nafasi na kushindwa kuonesha upinzani halisi kwa Saimoni Msuva au Haruna Niyonzima eneo la kati . Bado kijana mdogo ambaye akitumia vyema mapumziko haya kujijenga atafanikiwa lakini haraka ya mafaniko ya Yanga SC katika ligi inazoshiriki ni mtihani kwake . Lwandamina anahitajika pia kuangalia mbadala sahihi wa Saimoni Msuva ili kuleta ushindani halisi wa namba kikosini na kuiweka vyema timu katika uwiano mzuri wa wachezaji kikosini.
Safu ya ushambuliaji Lwandamina ana changamoto kubwa . Anapoikosa kombinesheni ya Donald Ngoma na Amisi Tambwe kikosi kinapwaya . Kama sio kupanda kwa kiwango cha Obrey Chirwa duru hili la pili la ligi kuu , Yanga ilikuwa katika hali mbaya katika eneo hilo. Kuumia kwa Donald Ngoma na Amisi Tambwe lilikuwa pigo kwa benchi la ufundi la timu hiyo na hii ilitokana kwa wachezaji kama Malimi Busungu kuikacha kambi na kuendekeza starehe na Mateo Antony kutokuwa katika ubora mzuri kuibeba timu. Upangwaji wa Obrey Chirwa kama mshambuliaji wa kati akizungukwa na viungo washambuliaji kama playmakers kwake ilisaidia kwa kiasi kikubwa .
Ni dhahiri katika ripoti yake George Lwandamina atalitazama vyema eneo hilo ili kuipa kasi timu katika ufungaji . Ni muda wa kujiuliza kuna haja ya kuendelea na baadhi ya wachezaji katika eneo hilo ? Au kuleta wapya wenye kasi na njaa ya mafaniko sio kama kina Malimi Busungu.
Lwandamina anahitajika kutulia na kukisuka kikosi vyema endapo atapata fungu zuri la usajili kipindi hiki cha mapumziko hususani kwa kuijenga timu hiyo kwa kutizama viwango vya timu ambazo atakutana nazo katika michuano ya klabu bingwa Afrika na sio ligi ya ndani.
Yanga SC imejikuta msimu huu ikiondolewa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika na sababu kubwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye viwango vya wastani kupambana kimataifa. Ni dhahiri kama wangekuwa na viwango bora wasingeondolewa na Zanaco FC kwa faida ya goli la ugenini .
Viwango vya wachezaji wa  Yanga SC na upambanaji kitimu kwa ujumla vilionekana vipo chini katika play off na MC Alger nchini Algeria . Usajili na ujenzi wa kikosi cha Yanga SC ulenge kushinda upinzani kama ule sio kuchukua alama tatu mbele ya Majimaji FC . Lwandamina huu ni wakati wake kuijenga Yanga mpya maana kikosi alichokikuta kwa asilimia 98 kilijengwa na Hans Van Pluijm
.

SERENGETI BOYS WAONDOKA LEO USIKU GABON

SERENGETI BOYS WAONDOKA LEO USIKU GABON


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ijulikanayo kwa jina la utani la Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka mjini hapa Saa 7.15 usiku wa leo kurejea nyumbani, Dar es Salaam baada ya kutolewa kwenye Fainali za Vijana Afrika juzi.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ambaye yuko na timu hiyo mjini hapa, amesema kwamba Serengeti Boys inatarajiwa kuingia Dar es Salaam Saa 8.50 mchana wa kesho na moja kwa moja kwenda kambini, hoteli ya Urban iliyopo katikati ya jiji kwa ajili ya kuagwa.
Beki wa kushoto wa Serengeti Boys, Nickson Kibabage akiwa amepigwa butwaa baada ya mechi Jumapili
Serengeti ilitolewa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Jumapili Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, Gabon.
Matokeo hayo yalizifanya Niger na Tanzania zifungane pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao akafuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Niger imeungana na Mali iliyoongoza kundi kwa pointi zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zimetolewa. Timu nyingine zilizofuzu Nusu Fainali ni Ghana na Guinea kutoka Kundi A. 

CHANZO BIN ZUBERY

SPORTPESA YAWAPA MILIONI 250 SINGIDA UNITED ZA UDHAMINI LIGI KUU

SPORTPESA YAWAPA MILIONI 250 SINGIDA UNITED ZA UDHAMINI LIGI KUU



KAMPUNI ya SportPesa leo imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Singida United kwa dau la Sh. Milioni 250.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema kwamba wameingia mkataba na timu hiyo kwa sababu imeonyesha nia ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao kutokana na usajili mzuri wanaoufanya.  
“Tumeingia mkataba na Singida United ambayo ndiyo timu ya mwisho katika udhamini wa SportPesa nchini, kutokana na timu hii kuwa na maandalizi mazuri,”amesema Tarimba.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia) akiwa na viongozi wa Singida United leo baada ya kusaini mkataba

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga, Tarimba amesema kwamba mkataba huo una kipengele cha kuongezwa iwapo Singida United itafanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya msimu ujao.
Kwa upande wake, kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba udhamini huo ni chachuya timu kufanya vizuri msimu ujao.
“Nafurahi baada ya mafanikio yangu nikiwa na Yanga, sasa Napata fursa nyingine nzuri ya kuendeleza mafanikio hayo na Singida United,”amesema.
Mchezaji wa Singida United, Nizar Khalfan akiwa na jezi yenye nembo ya SportPesa

CHANZO BIN ZUBERY

Uingereza imeanza rasmi kujitoa kwenye umoja wa Ulaya

Uingereza imeanza rasmi kujitoa kwenye umoja wa Ulaya

mediaRais wa tume ya umoja wa Ulaya, Donald Tusk, akipokea barua rasmi kumtaarifu Uingereza kuanza kutoka kwenye umoja wa Ulaya. Machi 29, 2017
Hatimaye Uingereza imeanza rasmi mchakato wa kutoka kwenye Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, ikisema “hakuna kurudi nyuma” kutokana na uamuzi ambao umeigawa nchi hiyo na kuibua maswali mengi kuhusu mustakabali wa jumuiya hiyo.
Ikiwa ni siku chache tu toka jumuiya hiyo iadhimishe miaka 60 ya uwepo wake, Uingereza imekuwa nchi ya kwanza kuondoka kwenye jumuiya ya nchi 28 wanachama, ikitoa pigo kwenye moyo wa ushirikiano wake toka kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
“Hii ni hatua ya kihistoria ambayo kamwe hakuna kurudi nyuma,” amesema waziri mkuu Theresa May wakati akiwahutubia wabunge Jumatano hii.
Miezi 9 baada ya hatua ya kushangaza ya Uingereza kupiga kura kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya, nchi hiyo imeanza kutekeleza hatua ya awali ya kutengua ibara ya 50 ya mkataba wa Lisbon, ikianza kuhesabu muda wa miaka miwili hadi kutamatisha utaratibu wa kuwa imejiondoa kabisa.
“Tayari tumewamisi,” amesema rais wa tume ya Ulaya Donald Tusk mjini Brussels baada ya kupokea barua rasmi kumtaarifu nia ya Uingereza kujitoa.
Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May. 29 Machi, 2017Parliament TV 
Hata hivyo rais wa Ufaransa ameonya kuwa kujiondoa kwa Uingereza kutakuwa na maumivu makali kwa Waingereza.
Umoja wa Ulaya umesisitiza kulinda umoja wake ambapo umeongeza kuwa kujitoa kwa Uingereza hakutashawishi nchi zaid kujiondoa.
Barua ya kurasa sita iliyotiwa saini na waziri mkuu May na kuwasilishwa kwa mkono na balozi wake kwenye umoja huo Tim Barrow jijini Brussels, imetaka kuheshimiwa na kuwa na ushirikiano wa heshima kati yao.
May kwenye barua yake amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwenye masuala ya usalama, akisema kushindwa kufikia makubaliano katika hili kutamaanisha kuwa ushirikiano kwenye vita dhidi ya ugaidi utadhoofika.
Waziri mkuu May amesisitiza nia yake ya kuanzisha ushirikiano mpya na umoja wa Ulaya katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
chanzo REUTERS.

BAADA YA MAKONDA KUZUNGUMZA NA KITUO CHA STAR TV GWAJIMA HUYOOO.



WATUMISHI WANNE BABATI-MANYARA WATIMULIWA KWA UZEMBE KAZINI


Image result for MJI WA BABATIBARAZA la Madiwani la halmashauri ya mji wa Babati kupitia Mkurugenzi wa halmashauri hiyo limewafukuza kazi watumishi wane (4) wa Serikali wa wilaya hiyo kwa makossa mbalimbali akiwemo mwalimu mmoja wa shule ya sekondari.

Akisoma taarifa ya maamuzi hayo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mohamedi Kibiki alisema kuwa halmashauri imefikia uamuzi huo kutokana na watumishi hao kukiuka maadili ya kazi kwa kutoroka kazini muda wa kazi na mmoja kugushi cheti cha kidato cha nne (4).

Kibiki aliwataja watumishi hao kuwa ni Asha Hamis Abadallah aliyekuwa mtendaji wa mtaa wa Oysterbay, kata ya Babati aaliyegushi cheti, Dawi L. Sumaye mtendaji wa mtaa wa Wang’boo kata ya Bonga ambaye hakuweza kufika kazini siku tano (5) mfululizo bila taarifa.

Wengine ni Josephat Kimario Afisa mifugo kata ya Babati mwenye ngazi ya daraja ‘A’ na Mwalimu Ephraim J. Yaawo, mwalimu wa leseni wa shule ya sekondari Kwaang’w wote wakiwa na kosa la kutofika kazini Zaidi ya siku tano (5) mfululizo bila taarifa.

Akizungumzia uamuzi huo Mwenyekiti Kibiki alieleza kwamba watumishi hao wamekosa nidhamu sehemu zao za kazi na kwamba nidhamu inahitajika kwa watumishi ili kuepuka misukomisuko kama hiyo na mingine ndani ya maeneo yao ya kazi.

“Hakuna anayependa kumfukuza mtu kazi ila ni sheria  ndiyo inatubana, maamuzi haya ni magumu sana lakini hayuna jinsi kama kamati tumekaa na tumeazimia kwa vifungu vya sheria, kumfukuza mtu kazi ni kumpa wakati mgumu sana kwani anakwenda kuanza maisha mengine ambayo hakuyategemea”, alisema Kibiki.

Aidha aliwaasa watumishi kuwa makini katika maeneo yao ya kazi na ajira zao kwa ujumla na kueleza kwamba kuwakosesha wananchi huduma za kijamii kunasababisha migongano na migogoro isiyo ya lazima.

“Niwaombeni sana watumishi mlio kwenye ajira kwasasa muwe makini hasa katika maeneo yenu ya kazi, ogopeni sana kutuhumiwa na wananchi ili kuepuka madhara kama haya yaliyowakuta wenzenu”, alisisitiza.

MANJI AIAGA YANGA RASMI,SANGA AKAIMU NAFASI YAKE.


MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji amethibitisha kujiuzulu Uenyekiti wa klabu hiyo kuanzia juzi na kumuachia Makamu wake, Clement Sanga akaimu.
“Ni taarifa yangu na inajieleza yenyewe,”amesema Manji akizungumza kuthibitisha barua inayosambazwa kama taarifa kwa vyombo vya Habari.
Manji aliingia Yanga mwaka 2006 kama mdhamini kupitia kampuni yake ya Lotto Kitita, lakini baadaye akawa mfadhili Mkuu wa klabu kabla ya kuwa Mwenyekiti.
Na Manji anaondoka Yanga wakati tayari klabu imepata udhamini wa kampuni ya SportPesa, jambo ambalo halitaifanya iyumbe kiuchumi.
Katika kipindi chake cha kuwa mfadhili na Mwenyekiti wa Yanga, Manji atakumbukwa kwa mengi – kubwa ni kuirejeshea hadhi na heshima klabu hiyo.
Alipoingia mwaka 2006 aliikuta klabu ipo dhoofu kiuchumi na haiwezi kushindana na mahasimu wao, Simba katika kuwania wachezaji bora ambao ndiyo mtaji wa kushinda mataji.
Wakati huo Yanga ilikuwa inasajili wachezaji ambao ama walikuwa wameachwa na timu zao, waliojipeleka wenyewe kwa mapenzi yao au waliopatikana kwa njia ya mchujo wa majaribio.
Lakini mara baada ya Manji kuingia Yanga, klabu hiyo ikaanza kusifika kwa kusajili wachezaji wa kigeni na wale nyota wa hapa nyumbani, ikiwa ni pamoja na kubomoa ngome ya mahasimu, Simba SC.
Mwaka 2009 fedha za Manji zilimtoa kipa kipenzi cha wana Simba Msimbazi, Juma Kaseja na desturi hiyo ikaendelea baadaye wakichukuliwa beki Kelvin Yondan na mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi.
Yanga iliipiku Simba ‘kimafia’ katika kumsajili beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Mbuyu Twite kutoka APR ya Rwanda, tu kwa jeuri ya fedha.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage alianza kuonekana akimsainisha Mbuyu mjini Kigali, lakini baadaye Mwenyekiti wa Usajili wa timu ya Jangwani, Abdallah Bin Kleb akaingia kwa ‘gia kubwa’ na kubadilisha mambo, Mbuyu akatua Jangwani.
Na ni katika kipindi hicho imeshuhudiwa Manji amewazima kabisa Simba na Yanga ikitawala soka ya Tanzania na kuzidi kujiongezea mashabiki na wapenzi.
Lakini migogoro haikukosekana pia wakati wa utawala wa Manji, ambayo wakati fulani iliiathiri timu mfano ule wa kutaka kumng’oa aliyekuwa Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga ulioiponza klabu ifungwe 5-0 na mahasimu, Simba Mei 6, mwaka 2012.
Mapema mwaka huu, Manji alikuja na mpango wa kutaka kujikodisha klabu kupitia kampuni aliyoisajili kwa jina la Yanga Yetu, lakini ukapata upinzani mkali na kuamua kuachana nao.  
Kabla ya kufikia maamuzi haya, Manji alipitia kwenye misukosuko na Serikali kuanzia Januari hadi Aprili, kwanza akikamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na baadaye akidaiwa kumiliki pasipoti mbili.
Hali hiyo ilisababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kiufadhili Yanga na kufanya wachezaji wakose mishahara kwa kipindi chote hicho kabla ya viongozi wenzake kuanza kufanya jitihada za kulipa taratibu.
Lakini kwa ujumla ni udhamini wa SportPesa ndiyo unakuwa mkombozi wa tatizo la kiuchumi la Yanga baada ya Manji kuondoka.